🌟 "Usawa Kijinsia na Haki za Kijinsia"
Habari kutoka kwa Sarafina Saimon Mgendi, mdau wa maswala ya jinsia. Katika sauti yake ya leo, Sarafina anatufundisha kuhusu tofauti kati ya Usawa Kijinsia (Gender Equality) na Haki za Kijinsia (Gender Equity). @sautihub @sarafina_saimon11
👉 Usawa Kijinsia: Kila mtu apate haki sawa, fursa sawa, na rasilimali sawa bila kujali jinsia. Mfano, mishahara sawa kwa kazi sawa na upatikanaji sawa wa elimu kwa wavulana na wasichana.
👉 Haki za Kijinsia: Rasilimali na fursa zigawiwe kulingana na mahitaji ya kila mtu, kuhakikisha pengo la kijinsia linaondolewa. Mfano, ufadhili wa masomo kwa wasichana katika sekta zinazotawaliwa na wanaume kama uhandisi.
📢 Wito wa Sarafina: Tudumishe elimu kuhusu haki na usawa wa kijinsia, tuvunje mitazamo potofu, na tugawane majukumu kwa haki, nyumbani na kazini.
🙌 Tukijenga jamii yenye usawa, tunajenga mustakabali bora kwa wote!
Comments