top of page

Mabadiliko ya Tabia Nchi yanaleta changamoto kubwa kwa wanawake na watoto wa kike, nguzo muhimu za familia na jamii.

Saitot Kelvin Joel

🔍 Nchini Tanzania, zaidi ya 65% ya wakazi wanategemea kilimo kama chanzo cha kipato na chakula. Hata hivyo, athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kama ukame, mafuriko, na kuongezeka kwa gharama za maisha zimeongeza mzigo mkubwa kwa wanawake, hasa katika kutafuta maji na kuni.


📉 Uzalishaji wa mazao umepungua kwa zaidi ya 30% katika maeneo yenye ukame, hali inayohatarisha usalama wa chakula. Wakati huo huo, magonjwa kama malaria na kipindupindu yameongezeka, yakiathiri hasa afya ya wanawake na watoto wa kike.


👩‍👧 Katika bara la Afrika, wanawake hutumia zaidi ya saa 40 kwa wiki kutafuta maji na kuni, hali inayowazuia kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kielimu.


💡 Suluhisho letu? Tushirikiane kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuwekeza kwenye mbinu endelevu za kilimo, uhifadhi wa mazingira, na upatikanaji wa nishati mbadala. Wanawake wanastahili kuwa mstari wa mbele kama mawakala wa mabadiliko.


✊🏽 Pamoja, tunaweza kuhakikisha wanawake na watoto wa kike wanapata fursa bora za maisha na maendeleo.




15 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page