top of page
Saitot Kelvin Joel

Jiandikishe na Ushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa!

🗳️ Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni fursa muhimu ya kuleta mabadiliko katika jamii yako!


Kama Tanzania Projects Organization, tunaamini kuwa kila raia ana jukumu muhimu la kuchangia maendeleo ya jamii yake kupitia kupiga kura. Hii ni haki yako ya msingi, na njia muhimu ya kujenga uongozi bora, uwajibikaji, na ushirikishwaji wa wananchi.


Jiandikishe kwenye Orodha ya Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 11 - 20 Oktoba 2024, na hakikisha unakuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyahitaji!


Kupitia programu zetu za Uongozi wa Vijana na Uhamasishaji wa Wananchi, tunawahamasisha vijana na jamii kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika michakato ya demokrasia. Ushiriki wako unaleta maana, na pamoja tunaweza kuijenga Tanzania yenye maendeleo na uwajibikaji bora.



11 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page