💡 Usichelewe, Jali Afya Yako! Dr. Gloria Fela, mtaalamu wa afya na mdau wa maendeleo ya jamii, anatukumbusha umuhimu wa kutafuta msaada wa kitabibu mapema pale unapohisi dalili zozote za ugonjwa. Hatua hii siyo tu kwamba inasaidia kuokoa maisha bali pia huzuia madhara kama magonjwa sugu, ukilema, na gharama kubwa za matibabu. @gloryfela @sautihub @tanzaniaprojects
Kujali afya yako ni hatua muhimu kuelekea maisha yenye ubora. Ujumbe huu unawahusu watu wa rika zote kila mmoja ana wajibu wa kutanguliza afya yake na ya wapendwa wake.
🔔 Changia kwa kushiriki ujumbe huu na uwahimize watu kutafuta huduma za afya mapema. Kwa pamoja, tunaweza kujenga jamii yenye afya bora! @gloryfela @sautihub @tanzaniaprojects
Comments